Sudan Kusini :Kumbukumbu ya John Garang

Image caption Sanamu ya Kumbukumbu ya John Garang

Leo ni miaka kumi imepita tangu kufariki kwa muanzilishi wa kundi la waasi wa SPLM nchini Sudan, John Garang ambaye aliaga dunia katika ajali ya helikopta.

Garang alishinda msituni kwa miaka mingi akipambana na serikali ya Sudan, ilikujitenga na kujitawala wenyewe.

Image caption Raia wa Sudan Kusini wanaoishi Kenya wakiadhimisha siku hii

Baadaye bwana Garang alitambuliwa kama Makamu wa Rais wa Sudan baada ya kukubaliana kusaini mkataba wa amani.

Hata hivyo Sudan Kusini ilitangaza uhuru wake mwaka 2011.

Image caption Kundi la kitamaduni likiwatumbuiza wageni

Harakati za kisiasa za Garang ni za kupigiwa mfano katika taifa hilo changa japo kwa sasa limesakamwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka baada ya tofauti kuibuka baina ya rais Salva Kiir na aliyekuwa naibu wake Riek Machar.

Vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya miezi ishirini vimezamisha matumaini ya raia wa taifa hilo kurudi nyumbani kwani wengi wao wamekuwa wakimbizi katika mataifa jirani.

Raia wa Sudan Kusini wanaoishi mjini Nairobi Kenya wamekuwa wakikumbuka kiongozi wao na mwanzilishi wa harakati za ukombozi bwana Garang.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mgogoro baina rais Kiir na mpinzani wake Machar imechochea mapigano

Hata hivyo, wengi wao wanahisi kuwa mgawanyiko kati ya viongozi wa taifa hilo ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu na wengine wengi kuachwa bila makao.

Mgogoro huo wa uongozi umetia dosari mafanikio ya mashujaa wa taifa hilo.

''Si vyema kutengana hata baada ya kujipataia uhuru, ni heri viongozi wetu wanaozozana kuungana ili tupate amani.'' Alisema raia mmoja wa taifa hilo.

Image caption Rais Salva Kiir akiongoza maadhimisho ya Uhuru

Viongozi wa Sudan Kusini wamepewa hadi tarehe 17 mwezi Agosti kuafikiana la sivyo jumuiya ya Kimataifa, itachukua hatua za haraka kurejesha amani katika taifa hilo.

Garang na wapiganaji wenzake walianzisha chama kinachotawala cha sasa cha SPLM.