Zimbabwe: Aliyemuua simba Cecil aomba radhi

Haki miliki ya picha
Image caption Daktari wa meno Walter Palmer ameomba radhi kwa kuua simba Cecil nchini Zimbabwe

Raia wa Marekani ambaye ni Daktari wa meno, Walter Palmer, anayeshtumiwa kwa kuua simba ambaye ndiye aliyekuwa nembo ya uhifadhi wa wanyama porini nchini Zimbabwe na kivutio kikubwa cha watalii ameomba msamaha kwa tukio hilo.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Maandamano yamefanyika nje ya makazi yake daktari Palmer

Daktari huyo wa meno na mtu mwenye uraibu wa uwindaji wa wanyama pori anasema anajuta kwa kuua simba huyo maarufu Cecil , lakini akasema alidhani alikua katika mawindo halali.

Daktari huyo amewaomba radhi wateja wake katika jimbo la Minnesota Marekani ,ambao hapo jana waliandamana kuonesha gadhabu yao kwa tukio hilo ambalo linatathminiwa iwapo ni uwindaji haramu ama halali.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Simba Cecil aliyeuawa na Daktari Palmer

Hatima yake itaamuliwa karibuni na ndiyo itakayotoa mwelekeo iwapo daktari Palmer atafunguliwa mashtaka au la.

Tayari wanaume wawili wanakabiliwa na mashtaka ya uwindaji haramu nchini Zimbabwe kwa kumsaidia daktari Palmer kutekeleza mauaji ya simba huyo maarufu nchini Zimbabwe.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Simba huyo,Cecil,alitegwa na kuuawa nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Hwange.

Simba huyo,Cecil,alitegwa na kuuawa nje kidogo ya mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Hwange.

Bwana Palmer aliwaambia wateja wake kuwa anajuta sana kwa tukio hilo barani Afrika haswa baada ya shinikizo kutoka kwa waandamanaji waliomfananisha na muindaji haramu nje ya makaazi yake huko Minnesota nchini Marekani .

Simba huyo anaaminika kuwa aliuawa Julai mosi lakini mwili wake uliokuwa ukioza ulipatikana majuzi tu.