Nigeria yateua General mpya

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rais wa Nigeria Mhamadu Buhari

Nigeria imemteua Generali mpya kuongoza kikosi cha kimataifa kilichoundwa kwa ajili ya kupamba na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Meja General Iliyasu Isah Abbah ataongoza kikosi hicho kitakachokuwa na askari takriban 9000 kutoka nchi tano.

Nigeria imemchagua General huyo mpya kwa lengo la kupambana na wanamgambo hao wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuwa na ofisi zake katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na wanatarajiwa kuendesha operesheni zake kikamilifu kuanzia mwezi ujao.

Nigeria na majirani zake wamekuwa wanajitahidi kupambana na wapiganaji wa Boko Haram ambao wameua watu wapatao elfu ishirini.