Ligi kuu England kuanza kutimua vumbi

Image caption Maandalizi ya michuano ya ligi kuu ya Uingereza

Zikiwa zimesalia siku chache kuanza kutimua vumbi kwa michuano ya Ligi kuu ya Uingereza, mabingwa wa ligi hiyo timu ya Chelsea inatarajia kuivaa Arsenal katika Mechi ya ufunguzi inayotambulika kama ngao ya jamii itakayopigwa siku ya jumapili katika uwanja wa Wembley jijini London.

Ligi hiyo inatarajia kuanza Augosti nane kwa michezo sita ambapo Manchester United itachuana na Tottenham katika uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford wakati Bournemouth watawakabili Aston Villa,Norwich city wakipepetana na Crystal palace ,Leicester city ,nyumbani king power kukipiga na Sunderland,Everton watachuana na Watford na Chelsea dhidi ya Swansea city.