Charity Shield:Arsenal yaibwaga Chelsea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chamberlain

Mabingwa wa kombe la FA Arsenal wameshinda kombe la Charity Shield kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuwashinda mabingwa wa ligi ya Uingereza Chelsea 1-0 katika uwanja wa Wembley.

Alex Oxlaide Chamberlain alifunga bao hilo la ushindi na mguu wake wa kushoto.

Ramires alishindwa kufunga bao la wazi kutoka krosi iliopigwa na Loic Remy huku Chelsea ikishindwa kuona lango la wapinzani wake kabla ya muda wa mapumziko.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mourinho

Eden Hazard alipiga juu ya goli alipokuwa amesalia na kipa kabla ya mkwaju uliopgwa na Oscar kutolewa nje na kipa Petr Cech.

Ni mara ya kwanza kwa kipa huyo wa zamani wa Chelsea kuokoa hatari baada ya dakika 68 kabla ya kuokoa kichwa cha Kurt Zouma.