Je, IAAF imeshindwa mujukumu yake?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Je, IAAF imeshindwa mujukumu yake?

Shirikisho la kimataifa la riadha IAAF linakabiliwa na madai ya kushindwa kukabiliana na visa vingi vya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu miongoni mwa wanariadaha

Hii ni baada ya uchunguzi ulioendeshwa na gazeti la Uingereza la Sunday Times na kituo cha habari cha Ujerumani cha ARD, baada ya taarifa zilizovuja za maelfu ya matokeo ya uchunguzi wa damu kutoka kwa shirikisho hilo.

Wataalamu waliochunguza ushahidi huo walisema kuwa theluthi moja ya medali katika mashindano ya kimataifa kati ya mwaka 2001 na 2012 zilishindwa na wanariadha ambao matokeo yao ya uchunguzi yalikumbwa na utata.

Hata hivyo IAAF imetetea jitihada zake za kupambana na matumizi ya madawa ya kusisimua misuli.