Wayahudi waandamana dhidi ya wanamgambo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Picha ya mtoto wa Kipalestina aliyechomeka hadi kufa

Maelfu ya watu nchini Israeli wameshiriki kwenye maandamano wakiitaka serikali kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya wayahudi wanaotajwa kuwa wanamgambo.

Waandamanaji katika mji wa Tel Aviv walionyesha uzalendo wao kwa familia ya mtoto Mpalestina ambaye aliuawa siku ya ijumaa wakati nyumba katika eneo la ukingo wa magharibi ilipochomwa moto na wayahudi wenye itikadi kali.

Maandamano mengine yalifanyika katika eneo kulikofanyika shambulizi siku ya alhamis ambapo watu sita walidungwa visu wakati wa mkutano wa wapenzi wa jinsia moja.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Israel

Wakati huo huo kijana Mpalestina ambaye alipigwa risasi na wanajeshi wa Israeli wakati wa maandamano ya siku ya ijumaa ameaga dunia.