Sudan Kusini yakubaliwa katika Olimpiki

Mwakilishi wa Sudan Kusini katika kamati ya Olimpiki Haki miliki ya picha s sudan olympics

Sudan Kusini imetambuliwa rasmi na kamati ya kimataifa ya Olimpiki na hivo kuruhusiwa kushiriki katika Olimpiki mwakani huko Rio de Janeiro.

Sudan Kusini ilipata uhuru miaka mine iliyopita, na hivo haikuwahi tarehe ya mwisho ya kuweza kuingia katika Olimpiki ya London ya 2012.

Mkimbiaji wa Sudan Kusini, Guor Marial, alishiriki chini ya bendera ya Olimpiki.

Wawakilishi wa Sudan Kusini walitokwa machozi nchi yao ilipokubaliwa kuwa mwanachama wa Olimpiki na kuwa mwanachama 206.