Soko la hisa la Ugiriki lafunguliwa

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Soko la hisa la Ugiriki

Soko la hisa nchini Ugiriki limefunguliwa muda mfupi uliopita, baada ya kufungwa kwa miezi mitano.

Biashara katika soko hilo la hisa ilisimamishwa kutokana na mzozo wa kifedha uliolikumba taifa hilo mwezi Juni, pale benki nchini humo zilipofungwa na masharti magumu kuwekewa taifa hilo, hasa kuhusiana na viwango vya fedha ambavyo raia wa Ugiriki wanafaa kutoa kwenye akaunti zao.

Lakini wawekezaji wa ndani ya nchi, watakabiliwa na ugumu fulani hasa baada ya masharti yaliyowekwa ili kuzuia kupanda kwa soko la mtaji.

Hawataweza kutumia pesa kutoka katika akaunti zao za benki kununua hisa, ila tu fedha ambazo wako nazo majumbani mwao.

Mwenyekiti wa chama wafanyibiashara na viwanda Constantine Michalos, ameiambia BBC kuwa, anatarajia bei ya hisa kushuka leo, lakini ameongeza kuwa kufunguliwa tena kwa soko hilo kutawanufaisha wafanyibiashara.