Yemen yakabiliana na waasi wa Houthi

Haki miliki ya picha epa
Image caption Yemen

Wanajeshi wa serikali wameanzisha mashambulio makali yenye lengo la kuwafurusha waasi wa Kihouthi kutoka eneo moja lililokuwa kituo cha wanajeshi wa anga huko mjini Aden.

Kuna ripoti kuwa waasi kadhaa waliuawa .

Kituo hicho muhimu kiitwacho Al Anad kilikuwa pia kikitumiwa na majeshi ya Marekani waliokuwa wakitumia ndege zisizo na rubani kuwalenga wanachama wa kundi la Al Qaeda walioko Yemen.

Waasi wa Kihouthi walikuwa wameteka kituo hicho hapo mwezi Machi.

Lakini katika siku za hivi karibuni majeshi ya serikali yakisaidiwa na ndege za kivita za Saudia yalifanikiwa kuyarudisha maeneo kadhaa kwa serikali huku waasi hao wakifurushwa.