Takriban watu 20 wapoteza maisha India

Haki miliki ya picha P Singh Harda
Image caption Treni zilipotea njia na kutumbukia mtoni

Treni mbili zimekosea njia huko nchini India na kutumbukia katika mto nchini India

Treni hizo za abiria zilitumbukia katika mto uliokuwa umefurika kufuatia mvua kubwa katika Jimbo la Madhya Pradesh.

Shirika la habari la Associated Press limemnunukuu mmoja wa waokoaji akisema kuwa wamehesabu maiti 20.

zaidi ya abiria 250 wameokolewa, baada ya mabehewa sita kutumbukia mtoni

Wakuu wa shirika la Reli la India wanasema ajali hiyo ilitokea usiku wa manane kuamkia jumatano.

Anil Saksena, ni msemaji Shirika la Reli la India, amesema Treni moja ilitoka katika njia yake huku nyingine ikifuatia nyuma yake katika njia ya kupishana, Treni zilipoteza mwelekeo kutokana na mafuriko.