Kesi ya Julius Malema yatupiliwa mbali

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Malema

Mahakama ya Afrika Kusini imetupilia mbali kesi ya mashtaka ya udanganyifu na ufisadi dhidi kiongozi wa upinzani Julius Malema.

''Kesi hiyo inafaa kutupiliwa mbali kutokana na kucheleweshwa kwake'',jaji aliamuru.

Bwana Malema alishtakiwa mwaka 2012 kwa mashtaka ya fedha chafu pamoja na ufisadi kuhusiana na kandarasi za serikali zenye thamani ya dola milioni 4.

Alikana mashtaka hayo na kusema kwamba yalishinikizwa kisiasa.

Bwana Malema alibuni chama cha Economic Freedom Fighters mwaka 2013 kufuatia kufurushwa kwake katika chama tawala cha ANC.

Ni mkosoaji mkubwa wa rais Jacob Zuma na amefanya kampeni dhidi ya ufisadi.