Kiongozi wa Taleban huko Qatar ajiuzulu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hakimullah Mehsud

Kiongozi wa ofisi ya kisiasa ya kundi la wapiganaji wa Taliban huko Qatar, amejiuzulu jambo linalothibitisha mgawanyiko ndani ya kundi hilo , kufuatia kifo cha kiongozi wao Mullah Omar.

Katika taarifa aliyoitoa , Syed Mohammad Tayab Agha, ameashiria sababu yake ya kujiuzulu ni hatua ya baadhi ya wafuasi wa kundi hilo kuficha habari za kifo cha Mullah Omar kilichotokea miaka miwili iliyopita.

Ameongeza kusema Taliban inafaa kushughulikia maswala yake yote kutoka Afghanistan, ikiwemo uteuzi wa kiongozi mpya.

Hakutaja moja kwa moja iwapo matamshi hayo yanamlenga kiongozi mpya Mullah Akhtar Mansour - ambaye alitajwa juma lililopita kuwa kongozi mpya katika mkutano ulioandaliwa na baraza tawala huko Pakistan.

Lakini amekariri kuwa ni vigumu kumtumikia kiongozi aliyechaguliwa nje ya Afghanistan.

Viongozi wengine wakuu wa Taliban wamesema kuwa hawakushauriwa katika uteuzi huo