Marufuku ya mitandao ya ngono India yaondolewa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Marufuku ya mitandao ya ngono India yaondolewa

Serikali ya India imeruhusu mitandao ya filamu za ngono kuwepo baada ya shinikizo kutoka kwa wananchi.

Serikali iliondoa marufuku iliyoweka dhidi ya mitandao 857 ya kupeperusha filamu za ngono.

Idara ya mawasiliano imewaeleza watoaji wa huduma za intaneti dhidi ya kufunga kurasa zisizokuwa na video za ngono zinazowadhalilisha watoto.

Waziri Ravi Shankar Prasad alikutana na maafisa wakuu siku ya jumanne na kutoa uamuzi huo.

Serikali imepinga kutekeleza hatua za kuweka mpangilio za kimaadili na kueleza kuwa inawalinda watoto dhidi ya kutazama picha hizo.

Mwezi julai, mahakama kuu iliishtumu serikali kwa kutofunga mitandao yenye picha za uchi za ngono zinazowahusisha watoto.

Hata hivyo, watoaji wa huduma za intaneti wametofautiana na serikali.

Image caption India ilikuwa imeweka amri hiyo kali ilikulinda maswali ya watoto wasidhulumiwe

Msimamizi wa kampuni za kutoa huduma za mtandao wa intanet amenukuliwa kwenye gazeti la Times of India akieleza wasiwasi wao kuhusu kuwajibishwa kukagua kurasa zenye ngono zinazowahusisha watoto.

Taarifa za uondoaji wa marufuku hiyo zimevutia hisia mseto kwenye mitandao ya kijamii nchini humo huku viongozi wa kisiasa wakipinga uamuzi wa serikali kuondoa marufuku.

Aidha Waziri Prasad ameitetea serikali kwa kusema kuwa wanaheshimu uhuru wa vyombo vya mawasiliano.