MH370:Uchunguzi wa kina waanza Ufaransa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchunguzi wa kina waanza Ufaransa

Watalamu kutoka Ufaransa, Malaysia na Australia wameanza kuchunguza mabaki ya bawa la ndege iliyopatikana juma lililopita likiwa limesombwa hadi ufukweni na maji ya bahari Hindi katika kisiwa cha Re-Union karibu na Madagascar.

Nia hasa ni kubaini iwapo mabawa hayo ni sehemu ya mabaki ya ile ndege ya Malaysia ya MH370, iliyotoweka.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Inaaminika kuwa mabaki hayo ni kipande cha bawa la ndege hiyo ya MH370

Mabaki hayo yamehifadhiwa katika kambi ya jeshi iliyoko katika mji wa Toulouse.

Wataalamu hao watachukua alama za rangi na alama nyingine yeyote ile itakayowasaidia katika utambuzi wa ndege hiyo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sehemu iliyoshikana na ndege pia inachunguzwa ili kujua ilimeguka kutoka wapi.

Sehemu iliyoshikana na ndege pia inachunguzwa ili kujua ilimeguka kutoka wapi.

Ndege hiyo ya MH370, ilitoweka angani mwezi Machi mwaka jana ikiwa na abiria 239 na wahudumu wa ndege.