Mlipuaji awuawa watu 15 msikitini Saudia

Image caption Saudia

Mlipuaji wa kujitoa mhanga amefanya shambulio katika msikiti mmoja huko Saudia na kusababisha vifo vya watu 15.

Shambulio hilo limelenga msikiti ulioko eneo la mji wa Abha, msikiti unaotumiwa sana na vikosi vya usalama nchini humo.

Haijabainika kundi gani limehusika na shambulio hilo lakini dhana imeelekezewa waasi wa kihouthi katika nchi jirani ya Yemen .

Vikosi vya Saudia ndivyo vilivyoisaidia serikali ya Yemen kwa kushambulia ngome za wa-Houti kwa ndege za kivita jambo lililopelekea kuwashinda nguvu waasi hao.