Nigeria yapanga kuunda silaha zake

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameiamuru wizara ya ulinzi kujenga uwezo wa taifa hilo kujitengenezea silaha zake, haya ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na afisi ya rais.

Rais Buhari ametaja kuwa jambo ''lisilokubalika'' kwa taifa hilo ''kutegemea sana mataifa mengine kupata zana muhimu za kivita,'' taarifa hiyo imesema.

"Wizara ya Ulinzi inapewa jukumu la kutoa mipango iliyo bayana ya kujenga kiwanda cha cha zana za kivita nchini Nigeria," Rais Buhari amenukuliwa akisema.