Hali ni tete Kabul mabomu yameua watu 41

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Hali ni tete Kabul mabomu yameua watu 41

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anaongoza kikao maalum cha usalama baada ya mashambulizi kadha ya kujitolea muhanga yaliyopelekea watu 41 kufa.

Mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, umekumbwa na milipuko kadhaa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maafisa wa usalama wameimarisha doria mjini Kabul

Miongoni mwa maeneo yaliyolengwa ni chuo cha maafisa wa polisi, ambapo mtu mmoja aliyekuwa amevalia sare za polisi alijilipua na kuwaua zaidi ya watu 25.

Washambuliaji hao pia walivamia kituo cha wanajeshi wa shirika la kujihami la NATO kilichoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kituo cha wanajeshi wa NATO kililengwa

Inadaiwa kuwa wawili kati ya washambuliaji hao waliuawa.

Mapema siku ya Ijumaa lori moja lililokuwa limetegwa bomu lililipuka karibu na afisi za serikali na kuwaua watu 15.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anaongoza kikao maalum cha usalama

Rais Ashraf Khan alisema kuwa mashambulizi hayo yalikuwa ni lengo la Wapiganaji wa Kiislamu wa Taliban kujaribu kuwasahaulisha watu misukosuko inayokumba kundi lao kufuatia tangazo la juma lililopita kuwa mwanzilisi wa kundi hilo,Mullah Omar,alifariki.