Mwanablogu mwengine auawa Bangladesh

Haki miliki ya picha Facebook
Image caption Mwanablogu mwengine auawa Bangladesh

Mwandishi mwengine ameuawa nchini Pakistan baada ya kuvamiwa na kupigwa na umati wa watu.

Watu walimshambulia mwanablogu huyo na kumkatakata kwa madai kuwa alikuwa akikufuru katika maandishi yake.

Niladri Chatterjee, aliyekuwa akitumia jina la Niloy Neel katika maandishi yake, alitoka katika jamii ya watu wachache ya Wahindu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mkewe alisema kuwa Bangladesh kwa wakati huu ni taifa lililoko mikononi mwa Waislamu wenye itikadi kali.

Aliuawa na kundi la watu walioingia katika nyumba yake kwa madai kuwa walitaka kupangisha chumba katika nyumba yake jijini Dhaka.

Alijulikana kwa kuandika taarifa za kutoamini kuwepo kwa mwenyezi Mungu na kwa kuwakosoa waumini waislamu wenye itakadi kali.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Mwanablogu mwengine auawa Bangladesh

Mkewe aliyesikitishwa na mauaji hayo alisema kuwa Bangladesh kwa wakati huu ni taifa lililoko mikononi mwa Waislamu wenye itikadi kali.

Bi Chatterjee anasema kuwa laiti serikali ingetaka kuwepo kwa uhuru wa kujieleza ingeliwaadhibu waliomwua mumewe.

Hata hivyo Asha Moni alisisitiza kuwa wao pia wana haki ya kuishi nchini humo licha ya imani zao kinzani na ya waliowengi.