Chile: Raia washangilia kifo cha jemedari

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chile: Raia washangilia kifo cha jemedari

Mamia ya raia wa Chile wamejitokeza mabarabarani kushangilia habari za kifo cha jenerali Manuel Contreras,aliyekuwa kiongozi mkatili akisimamia shughuli za ujasusi wakati wa utawala wa Augusto Pinochet, nchini Chile

Manuel Contreras - aliyekuwa kiongozi mkatili akisimamia shughuli za ujasusi wakati wa utawala wa Augusto Pinochet, nchini Chile, ameaga dunia.

Contreras alikuwa amelazwa akiwa mahututi katika hospitali moja ya kijeshi jijini Santiago.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Contreras alikuwa amelazwa akiwa mahututi katika hospitali moja ya kijeshi jijini Santiago.

Madaktari walisimamisha shughuli zote za matibabu kwa Jemedari huyo, ambaye ana umri wa miaka 86.

Umati ulikusanyika nje ya hospitali ya kijeshi alikokuwa amelazwa.

Jemedari huyo aliyeongoza kikosi cha kijasusi wakati wa utawala wa Pinochet alikuwa amehukumiwa zaidi ya miaka 500 gerezani kwa ukiukaji wa haki za kibindamu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Makumi ya maelfu ya watu waliuawa wakati wa utawala wa Augusto Pinochet

Familia za waathiriwa wa ukatili chini ya utawala wa Pinochet, ulioshirikisha mauaji, kutoweka kwa wahusika na wapinzani wa wake na mateso ya miaka ya 70 na 80 ilisimamishwa na shirika la kijasusi lililosimamiwa najemedari huyo likijulikana kama DINA.

Jemedari Contreras alikuwa mwanzilishi wa kundi lililojulikana kama Plan Condor, lililosimamia shughuli zote za kisiasa na kikosi maalumu kilichokuwa na wajibu wa kuwaua watu waliodhaniwa kuwa maadui wa serikali.

Makumi ya maelfu ya watu waliuawa na kundi hilo.