Trump aanza kususiwa sababu ya ujuba

Donald Trump (katikati) katika mjadala uliooneshwa kwente televisheni  Alkhamisi Haki miliki ya picha AFP

Jukwaa maarufu la mrengo wa kulia (conservative) la Marekani limefuta mualiko wake kwa Donald Trump kuzungumza katika shughuli muhimu ya Jumamosi usiku.

Imesema sababu ni kuwa haikubaliki kwa Bwana Trump kusema kuwa mwandishi wa habari alimuuliza maswala magumu, kwa sababu alikuwa anapita siku zake za mwezi.

Ijumaa, Bwana Trump alisema kuwa Megyn Kelly wa shirika la utangazaji la Fox News "akitokwa damu machoni na kwengineko", baada ya mwandishi wa habari huyo kumuuliza swala la kumpinga katika mjadala uliooneshwa kwenye televisheni.

Shirika la mrengo wa kulia la Red State lilisema Bwana Trump alikuwa kama anadokeza kuwa Megyn Kelly alikuwa anasumbuliwa na homoni.

Megyn Kelly amealikwa katika shughuli ya Jumamosi kuzungumza badala ya Donald Trump.

Donald Trump ni mmoja kati ya watu kadha wanaoania kuchaguliwa kuwa mgombea urais wa chama cha Republican.