Msovieti aliyeiongoza Taliban kizimbani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Irek Hamidullin alipokamatwa na wanajeshi wa Marekani 2009

Jopo la wazee wa mahakama katika jimbo la Virginia, Marekani, limemkuta na hatia kamanda wa zamani wa jeshi la Sovieti, ya kuongoza shambulio la Taliban, dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan mwaka 2009.

Irek Hamidullin, ambaye alibadilisha dini na kuwa muislamu, alikabiliwa na mashtaka 15, pamoja na kuwasaidia magaidi, kujaribu kuangamiza ndege ya jeshi la Marekani, na njama ya kutumia silaha za kungamiza.

Adhabu ya baadhi ya mashtaka hayo ni kifungo cha maisha jela.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mawakili wanasema sio kitu cha kawaida, kwa mtu aliyetekwa vitani nchini Afghanistan, kupelekwa Marekani kushtakiwa

Mawakili wanasema sio kitu cha kawaida, kwa mtu aliyetekwa vitani nchini Afghanistan, kupelekwa Marekani kushtakiwa.

Mawakili wa mshtakiwa walidai, ingawa walishindwa, kwamba Hamidullin kimsingi ni mfungwa wa vitani, na haifai kumfikisha mbele ya mahakama ya raia.