Uchaguzi wa Haiti wafanyika miaka 4 baadaye

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uchaguzi wa Haiti wafanyika miaka 4 baadaye

Wananchi wa Haiti wanashiriki kwenye uchaguzi wa wabunge leo.

Uchaguzi huu uliahirishwa miaka minne iliyopita.

Wagombea zaidi ya 1,800 , kutoka vyama vingi vya kisiasa , wanawania viti vya ubunge.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bunge la taifa mjini Port-au-Prince, lilifutwa mwezi wa Januari

Uchaguzi huo unaonekana kama ishara ya utulivu katika nchi hiyo maskini.

Bunge la taifa mjini Port-au-Prince, lilifutwa mwezi wa Januari, kwa sababu ya kushindwa kufanya uchaguzi.

Tangu wakati huo Rais Michel Martelly ameongoza nchi hiyo kwa amri yake.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais mpya atachaguliwa mwezi Oktoba

Rais mpya atachaguliwa mwezi Oktoba.

Bwana Martelly mwenyewe haruhusiwi kushiriki uchaguzi huo