Nagasaki yakumbuka bomu iliyoua watu elfu 70

Haki miliki ya picha AP
Image caption Nagasaki yakumbuka bomu iliyoua watu elfu 70 miaka 70 iliyopita

Ibada maalumu za ukumbusho zinaendelea kufanywa katika mji wa Nagasaki, nchini Japan, kuadhimisha miaka 70 tangu kulipuliwa kwa bomu ya atomiki jijini humo.

Katika ibada hiyo mzee mmoja aliyenusurika aliibua hisia baada ya kukashifu hatua ya serikali iliyokomadarakani kwa kubadili vipengee vya katiba ya nchi hiyo ilikuruhusu wanajeshi wake kushiriki katika vita.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Manusura wa bomu hiyo ya Nyuklia iliyoua zaidi ya watu laki mbili

Maelfu ya watu waliohudhuria ibaada hiyo ya ukumbusho walimpigia makofi kwa uwazi wake.

Meya wa mji wa Nagasaki naye alivutia waya huohuo akimkashifu waziri mkuu bwana Shinzo Abe kwa jitihada za kubadilisha katiba ya nchi.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wazungumzaji wamekashifu hatua ya serikali iliyokomadarakani kwa kubadili vipengee vya katiba ya nchi hiyo ilikuruhusu wanajeshi wake kushiriki katika vita.

Bwana Abe alikaa kimya kando tu jukwaani.

Bomu hilo lilidondoshwa na wanahewa wa Marekani, siku tatu tu baada ya kudondosha lingine la kinukilia katika jiji la Hiroshima.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bomu hilo lilidondoshwa na wanahewa wa Marekani, siku tatu tu baada ya kudondosha lingine la kinukilia katika jiji la Hiroshima.

Bomu hilo liliangamiza kabisa mji huo na kuua watu zaidi ya 70,000 .

Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 200,000 waliuawa katika milipuko hiyo miwili, na wengine kufariki baadaye kutokana na miale ya sumu kutoka kwa mabomu hayo ya nguvu za kitonaradi.