Michael Brown akumbukwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michael Brown akumbukwa Ferguson

Huko Marekani,mamia ya watu walisimama kimya kwa muda wa dakika nne na nusu kwa pamoja mjini Ferguson ,missouri sehemu ambayo kijana asiye na hatia Michael Brown aliuwawa na polisi mmoja wa kizungu mwaka mmoja uliopita.

Ishara hiyo inaashiria muda ambao mwili wake ulilala katikati ya barabara bila kupata msaada wowote.

Njiwa wawili walipeperushwa hewani na watu waliandamana kimya kimya ili kutoa heshima kwa Michael Brown na wengine ambao walikufa katika mikono ya polisi.

Mauaji hayo yalileta mjadala dhidi ya ubaguzi wa polisi nchini Marekani na ulimwenguni.