Wahouthi taabani huko Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Majeshi ya muungano yamewabana wapiganaji waasi katika mji wa Zinjibar

Mapigano makali yanaendelea Kusini mwa Yemeni kati ya majeshi yaliyo na imani na serikali yanayotaka kuwatimua waasi wa Kihuthi wanaoungwa mkono na Iran wanaokalia maeneo kadhaa ya nchi hiyo. Wanajeshi waaminifu kwa serikali wakikomboa mji mkuu wa Abyan, itakuwa pigo kubwa kwa waasi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Muungano wa wanajeshi wanaoongozwa na Saudi Arabia wamewabana Wahouthi

Waasi hao wamepunguzwa makali kufuatia kushindwa mara kadhaa na muungano wa wanajeshi wanaoongozwa na Saudi Arabia.

Habari kutoka Himarati zinasema kuwa wanajeshi watatu wa himaya hiyo waliuawa katika mapigano ya jumamosi.

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Wahouthi taabani huko Yemen

Wanajeshi wa muungano wa mataifa ya Kisunni wamekuwa wakipigana na Wahuthi hao ambao ni Wasunni, kwa lengo la kurejesha mamlakani utawala wa serikali ambayo kwa hivi sasa imetimuliwa katika makao makuu ya nchi.