Muhammadu Buhari kupambana na rushwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameteua kamati itakayomshauri njia sahihi ya kupambana na rushwa sambamba na kupata mfumo mzuri wa sheria nchini humo.

Walioteuliwa katika kamati hiyo wengi wao ni wasomi wakubwa nchini Nigeria. Msemaji wa Rais hakutamka wazi ni lini wangeweza kuja na matokeo sahihi ya kile wanachokitaka.

Rais Buhari aliyechaguliwa mwezi Mei mwaka huu akiwa na ahadi ya kupambana na rushwa, hapo awali alitamka wazi kuwa anaamini maafisa wa serikali wameiba zaidi ya dola bilioni hamsini kutoka mfuko wa fedha za umma kwa zaidi ya muongo mmoja.