Burundi:Waliomuua jenerali Nshimirimana wakamatwa

Haki miliki ya picha no credit
Image caption Waliomuua jenerali Nshimiriman wakamtwa

Kiongozi wa mashtaka nchini Burundi amesema kuwa watu kadhaa wanaoshukiwa kutekeleza mauaji ya jenerali Adolphe Nshimirimana wamekamatwa

Hata hivyo Afisa huyo anasema kuwa viongozi waliopanga njama ya kumua jenerali huyo wangali wanasakwa.

Image caption Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi

Kufuatia mauaji ya kiongozi huyo wa kikosi cha ulinzi wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Mwanaharakati maarufu wa haki za kibinaadamu nchini humo alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na watu waliokuwa katika pikipiki .

Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mapema wiki hii .

Mbonimpa amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.

Haki miliki ya picha
Image caption Nkurunziza alishinda uchaguzi mkuu mwezi uliopita uliosusiwa na upinzani.

Hadi kufikia sasa haijajulikana ni nani aliyekuwa amelenga kumtoa uhai.

Wakati huohuo taharuki imetanda katika mji mkuu wa Bujumbura baada ya milio ya risasi kusikika katika maeno kadha ya mji huo usiku wa kuamkia leo.

Hakuna taarifa zaidi ila habari zinasema huenda wanajeshi kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa.

Inaelezwa milio hiyo ya risasi ilisikika baada ya gari moja kutoka ofisi ya Rais wa nchi hiyo kuchomwa moto.

Haki miliki ya picha
Image caption Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu.

Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu.

Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.

Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.