Francois Bozize asema atarudi CAR

Haki miliki ya picha AP
Image caption Bozize

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya kati Francois Bozize ambaye kwa sasa yuko mafichoni amesema kwamba huenda akarudi nchini humo ili kuwania urais mwezi Octoba.

Chama chake cha KNK kimemteua yeye licha ya kutokuwepo wiki iliopita kuwa mgombea wake.

''Nitarudi CAR haraka iwezekanavyo iwapo hakuna matatizo yoyote. Lakini inaonekana kwamba mamlaka nchini hayataki kuniona'',aliiambia BBC Afrique.