Uchumi wa Urusi wayumba

Takwimu za serikali ya Urusi kuhusiana na uchumi wa nchi hiyo zinaonesha kuporomoka kwa asilimia nne nukta sita katika robo ya pili ya mwaka huu wa 2015 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Takwimu za awali zinaonyesha juhudi za kuuinua uchumi zikiwa zimeshindikana ikilinganishawa na vipindi vya nyuma. Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanasema kuwa takwimu hizo ni mbaya zaidi kuliko ambavyo serikali ya Urusi ilivyotarajia huku mtikisiko ukiendelea kuwa mkubwa unaosababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta pamoja na vikwazo kutoka nchi za Magharibi vinavyotokana na mgogoro wa Ukraine.

Uchumi wa Urusi unasemekana pia kuathiriwa zaidi na ukosefu wa ajira unaosababisha uhitaji wa chini kwa walaji na kuporomoka kwa uzalishaji.