Wanaowaajiri wahamiaji haramu kuadhibiwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji haramu

Biashara zinazoowaajiri wahamiaji haramu zitachukuliwa hatua kali kulingana na waziri wa uhamiaji nchini Uingereza.

Akitangaza mwelekeo mpya kwa waajiri wasiotii sheria ambao huwaajiri wahamiaji haramu,amesema kuwa wanawanyima kazi raia wa Uingereza na kushusha viwango vya mishahara.

Maafisa wa Uhamiaji wanadaiwa kutayarisha uvamizi kwa lengo la kuwanasa wafanyibiashara hao katika sekta kadhaa.

Gazeti la the times linasema kuwa kampuni za kufanya usafi ,zile za mijengo pamoja na nyumba za kuwauguza watu zitalengwa.

Mwandishi wa BBC Robin Brant amesema kuwa mawaziri wanajaribu kuweka mikakati ya kukabiliana na wafanyikazi haramu badala ya kubuni sheria mpya.