Google yajiimarisha kupitia Alphabet

Haki miliki ya picha AP
Image caption Afisa mkuu wa Google Sundar Pichai

Kampuni ya Google imeanzisha kampuni nyengine kwa jina Alphabet.

Katika hatua yake ya kujiimarisha zaidi Google itaendelea kusimamia biashara zake kama vile programu,You Tube na Android.

Lakini idara zake mpya kama vile ile ya uwekezaji pamoja na utafiti ,smart-home',unit test na drone arm zitasimamiwa na kampuni hiyo ya Alphabet.

Mwanzilishi wa Google, Larry page amesema kuwa atabuni mfumo rahisi utakaoendesha biashara hiyo inayozidi kupanuka.

''Mfumo huo mpya utatuwezesha kuangazia vyema fursa zilizopo katika kampuni ya google'',alisema katika blogi yake.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Google

''Kampuni yetu inaendelea vyema leo,lakini tunadhani kwamba tunaweza kuisafisha na kuifanya kuwajibika zaidi,alisema.

''Swala muhimu ni kwamba kampuni zitakazosimamiwa na Alphabet zitakuwa na uhuru wa kuendeleza bidhaa zake''.

Bwana Page atakuwa mkurugenzi mkuu wa Alphabet,huku makamu wake wa rais Sundar Pichai akiwa afisa mkuu wa Google.