Bunge la Iraq launga mkono marekebisho

Image caption Bunge la Iraq

Bunge la Iraq limepiga kura kwa wingi ili kuunga mkono mapendekezo yaliotolewa na waziri mkuu Haider al Abadi ,kwa lengo la kukabiliana na ufisadi pamoja na kupunguza matumizi ya serikali.

Spika wa bunge hilo Salim al Juburi amesema kuwa mswada huo umepitishwa bila upinzani wowote.

Mpango huo unashirikisha kupunguzwa kwa baadhi ya nyadhfa serikalini ,kumaliza ubaguzi wa kidini pamoja na ule wa kisisasa wakati wa kutolewa kwa ajira serikalini mbali na kuanzisha uchunguzi dhidi ya ufisadi.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kumekuwa na maanadamano ya raia kuhusu kukatizwa mara kwa mara kwa umeme wakati ambapo kuna joto jingi mbali na ufisadi serikalini pamoja na uzembe.