Uturuki kuwalinda wahamiaji

Haki miliki ya picha hurriyet.com.tr
Image caption Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu

Waziri mkuu wa Uturuki Ahmet Davutoglu, amesema nchi yake ina nia ya kuanzisha eneo salama kwa ajili ya raia wanaovuka mipaka ya kaskazini mwa Syria, kwa msaada wa Marekani na nchi nyingine.

Akihojiwa na BBC amesema kile anachokiita makundi ya waasi ya Syria yamekua yakiwashambulia raia hao ama kwa vikosi vya Rais Assad pamoja na IS. Lakini msemaji wa mambo ya nje wa Marekani Mark Toner Alisema Washington ilikuwa inazungumzia juu ya jitihada endelevu za kuwaondoa IS katika eneo hilo .