Thamani ya Yuan yapunguzwa tena

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Thamani ya sarafu ya Yuan yashukishwa tena

Uchina kwa mara nyengine imepunguza thamani ya sarafu yake, Yuan, ikilinganishwa na dola, kwa siku ya pili mfululizo.

Hatua hiyo imeshtua masoko ya hisa kwa kuwa Yuan sasa imeshuka kwa kiwango cha chini sana kwa muda wa miaka minne.

Mnamo Jumanne Uchina ililazimika kuchukua hatua ya kupunguza gharama ya Yuan kwa asilimia mbili ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi zina bei ya ushindani katika soko la kimataifa.

Hii leo gharama ya Yuan imepunguzwa kwa asilimia moja nukta sita.

Sarafu zingine za bara la Asia zimevurugika, kutokana na wasiwasi wa mataifa mengine yaliyo jirani na Uchina yanayoshuku hali ya uchumi wa Uchina.