Moto mkubwa wazuka Tianjin-China

Haki miliki ya picha
Image caption Mji wa viwanda ukiteketea

Kumetokea mlipuko mkubwa katika mji wa China Tianjin-ambao ni mji wa Bandari kuu na sehemu ya viwanda katika eneo la kusini kaskazini mwa mji mkuu Beijing.

Video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha moto mkubwa na wingu kubwa la moshi lililotanda angani. Shirika la habari la nchi hiyo, Xinhua limesema mlipuko huo umetokea katika mji wa Tianjin Binhai ukanda ulioendelea kiviwanda uliopo karibu na bandari na watu wanakimbia katika eneo hilo kunusuru maisha yao.Mpaka sasa bado hakijajulikana chanzo kikuu cha moto huo ni nini.