Daniel Ceballos ameachiliwa huru

Image caption Daniel Ceballos

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Venezuela Daniel Ceballos ameachiliwa kutoka kifungoni na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani.

Hakimu alisema kuwa bwana Ceballos anakabiliwa na matatizo ya kiafya yanayomfanya ashindwe kuendelea kubaki gerezani.Ceballos Alikamatwa machi mwaka jana kwa tuhuma za kuchochea vurugu wakati wa maandamano dhidi ya uhaba wa chakula, mfumuko wa bei pamoja na kukithiri kwa uhalifu.

Bwana Ceballos ni kiongozi wa pili wa upinzani kuachiliwa huru mwaka huu (baada ya Antonio Ledezma mwezi Aprili ambaye ni meya wa zamani wa San Cristobal, ulipo Magharibi mwa ngome kuu ya upinzani nchini humo.

zaidi ya watu arobaini walifariki dunia katika maandamano hayo kutoka pande zote mbili zenye mgawanyiko wa kisiasa