Jimmy Carter asema ana kansa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jimmy Carter Rais wa zamani wa Marekani

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter ametangaza kuwa ana maradhi ya kansa. Carter mwenye umri wa miaka tisini ,na siku za hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa ini.

Jimmy amesema kuwa imebainika kuwa ana kansa ambayo imekwisha sambaa katika baadhi ya sehemu za mwili wake. Ameongeza kuwa yupo katika mpango wa kuweka vizuri ratiba yake kwa lengo la kupata matibabu zaidi.

Jimmy Carter toka aondoke madarakani ,amekua akijisughulisha na kazi za kuhudumia jamii duniani kote.