Syria:Makubaliano ya amani yatekelezwa

Haki miliki ya picha afp
Image caption Syria mazungumzo

Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 48 yameanza kufanya kazi kati ya muungano wa waasi Syria na vikosi vinavyoiunga serikali mkono katika miji mitatu.

Makubaliano hayo ya muda yamenuiwa kuruhusu kusafirishwa kwa chakula na dawa katika eneo linalodhibitiwa na waasi la Zabadani katika mpaka na Lebanon na katika vijiji viwili kaskazini magharibi mwa nchi inayodhibitiwa na jeshi la Syria.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema kuongezeka kwa wanajeshi katika eneo hilo kunaonekana kusababisha majadiliano katika eneo hilo.

Shirika linalotetea haki za binaadamu Syria limesema makubaliano hayo yaliafikiwa kati ya serikali na vikosi vinavyoiunga Iran mkono na kwa upande wa waasi na Ahrar Al-Sham, mshirika wa kundi la Al Nusra Front.