Kiongozi wa Al Qaeda kumtii mkuu wa Taliban

Haki miliki ya picha AP
Image caption al-Zawahiri kumtii Mullah Akhtar Mansour

Kiongozi wa Al-Qaeda Ayman al-Zawahiri amekula kiapo kumtii kiongozi wa wapiganaji wa kiislamu wa Taliban nchini Afghanistan.

Habari hizo zimeibuka baada ya sauti yake akikariri uaminifu wake kwa kiongozi huyo kuchapishwa kwenye mitandao.

Kauli hiyo ya uaminifu kwa Mullah Akhtar Mansour iliachiliwa kwenye mitandao na kitengo cha habari cha Al-Qaeda, Al-Sahab.

Hii vilevile ndiyo ripoti ya kwanza ya al-Zawahiri tangu alipotoa ripoti yake ya kwanza mnamo mwezi septemba mwaka uliopita.

Kumekua na ati ati iwapo al-Zawahiri yuko hai au aliaga dunia sawa na mtangulizi wake ambaye alikuwa kiongozi wa kundi hilo la Taliban Mullah Omar.

Kifo cha Mullah kilithibitishwa mwezi uliopita.

Zawahiri katika taarifa hiyo mpya anatuma rambirambi kufuatia kifo cha Mullah Omar.