Uchumi wa Ugiriki umekuwa 1%

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uchumi wa Ugiriki umeshangaza kwa kuonyesha dalili za ukuwaji.

Uchumi wa Ugiriki umeshangaza kwa kuonyesha dalili za ukuwaji.

Takwimu rasmi za hivi karibuni zinaashiria uchumi umepanuka kwa takriban asilimia moja katika robo ya pili ya mwaka.

Hiyo ilikua ni kabla ya kuporomoka kwa mazungumzo ya mkopo kuhusu mzozo wa kifedha wa nchi hiyo na kufungwa kwa benki zake.

Bunge huko Athens linajitayarisha kupiga kura kuamua kuhusu mpango mpya unaokumbwa na mzozo wenye thamani ya euro bilioni 85 ili kwa upande mwingine serikali iidhinishe hatua kali za kubana matumizi na kuongeza kodi.

Image caption Hiyo ilikua ni kabla ya kuporomoka kwa mazungumzo ya mkopo

Upinzani umeahidi kuunga mkono mpango huo, baadhi ya wabunge wa mrengo wa kushoto katika chama tawala Syriza wanasema ni lazima kutimize ahadi yake ya kupinga hatua za kubana matumizi.