Polisi wavamia Chama cha Wanajeshi Myanmar

Haki miliki ya picha AP
Image caption Polisi wavamia Chama cha Wanajeshi Myanmar

Polisi na wanajeshi wa Myanmar wamevamia makao makuu ya chama kinachoungwa mkono na jeshi cha Nay-Pyi-daw.

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa lakini waandishi wa habari katika eneo hilo wamesema kuwa hali ya sintofahamu katika chama hicho imesababishwa na ushindani mkali wa kung'ang'ania madaraka katika chama hicho kinachotawala miezi kadhaa iliyopita.

Na habari zinazotufikia hivi sasa ni kuwa Spika wa Bunge la Myanmar ameondolewa kama mwenyekiti wa chama kinachotawala miezi mitatu kabla ya uchaguzi Mkuu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sintofahamu katika chama hicho imesababishwa na ushindani mkali wa kung'ang'ania madaraka

Mndani wa chama hicho ambaye hakutaka kujulikana alisema kuwa spika huyo ameondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na mtu asiyependelea mabadiliko ajulikanaye kama Thein Sein.