Marufuku ya tambi za Nestle yaondolewa India

Image caption Mahakama moja nchini India imeondoa marufuku dhidi ya tambi za Nestle

Marufuku ya tambi za kampuni ya kutengeneza chakula ya Nestle imeondolewa.

Mahakama moja India imetoa uamuzi kwa manufaa ya kampuni ya kimataifa ya kutengeneza chakula Nestle kuhusu kupigwa marufuku tambi zake- Maggi.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Marufuku hiyo sasa imeondolewa kwa wiki sita

Marufuku hiyo sasa imeondolewa kwa wiki sita kukisubiriwa ukaguzi mpya wa tambi hizo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption tambi hizo zilipigwa marufuku kwa sababu zilikuwa na kiwango cha juu cha risasi (Lead)

Nestle iliagizwa kuondosha tambi hizo za Maggi kutoka soko la India baada ya ukaguzi uliofanywa katika baadhi ya majimbo kugunduwa kuwa zina kiwango kikubwa cha madini ya Lead. Uamuzi huo unajri siku moja baada ya serikali ya India kusema inawasilisha kesi dhidi ya Nestle kutaka iilipe serikali takriban dola milioni mia moja kwa hasara.