Ugiriki yajitathmini na madeni kimataifa

Kumekuwa na majadiliano makubwa katika bunge la Ugiriki kuhusu mdahalo wa kama wabunge wataunga mkono suala la nchi hiyo kuokoa uchumi wake kwa mara ya tatu.

Mpango huo wenye thamani ya Euro bilioni themanini na tano,utaendana na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima sambamba na kuongezeka kwa kodi. Takwimu kadhaa kutoka upande wa mrengo wa kushoto zinasema serikali inakaidi viongozi wake wenyewe huku zikisema ahadi yao ni kupambana na uongozi mbaya.

Wadadisi wanasema kuwa kuna uwezekano seikali ikashinda kura inayotarajiwa kupigwa, lakini kwa msaada wa wabunge wa upinzani,mdahalo huo umekuja kutokana na takwimu mpya kuonyesha kua kwa kiasi fulani,uchumi wa Ugiriki umeongezeka kwa asilimia moja katika robo ya pili ya mwaka huu bila kutarajia.