Japan inajutia vita vya pili vya dunia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, ameeleza kusikitishwa kwake na mateso na kujitolea kwa watu wengi wakati wa vita vya pili vya dunia.

Katika hotuba aliyotoa kuadhimisha miaka 70 tangu kushindwa nchi yake katika vita hivyo, Abe ameeleza alichokitaja kuwa kujutia makosa yaliofanywa dhidi ya wanawake ambao walinyimwa heshima zao wakati wa vita.

Amesema Japan inapaswa kuhakikisha kwamba mzozo wa aina hiyo hautokei tena.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manusura wa vita vikuu vya pili vya dunia mjini Hong Kong wameandamana wakitaka fidia

Bwana Abe ameitoa kauli hiyo wakati wa sherehe za maadhimishisho ya miaka sabini tangu Japan iliposhindwa vita hivyo

Wakati huo huo kundi la manusura wa vita vikuu vya pili vya dunia mjini Hong Kong wamefanya maandamano nje ya ubalozi mdogo wa Japan kudai fidia kwa kupoteza pesa ambapo wanasema walipata shida kutokana na Japan kuuvamia na kuuteka mji wao .

Haki miliki ya picha
Image caption Hotuba hiyo ilikuwa ya kuadhimisha miaka 70 tangu kushindwa nchi yake katika vita hivyo

Waandamanaji hao wanataka Japan iwabadilishie pesa zao za noti za benki ambazo haitumiki kwa sasa , iwapatie pesa halali .

Wakati wa uvamizi wa Japan wakazi wa Hong kong walilazimishwa kutumia pea zinazofahamika kama YEN za kijeshi mbazo hazikuwa na thamani baada ya vita .