Israel:Mpalestina aliyesusia chakula yu mahututi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mamake Allaan alipohudhuria maandamano ya kutaka aachiliwe huru

Mfungwa wa Palestina nchini Israel ambaye amesusia chakula kwa takriban siku 60 amepoteza fahamu.

Mohammed Allaan amekataa kula akilalamikia kufungwa kwake kwa takriban miezi tisa sasa pasi na kukabiliwa na shtaka lolote.

Allaan kwa sasa anapata usaidizi wa mashini kupumua hospitalini na watetezi wa haki za binaadamu huko Upalestina wametaka hatua za dharura zichukuliwe kuokoa maisha yake.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Allaan alizuliwa katika gereza la Israel kwa kuhusishwa na kundi la kiislamu la Islamic Jihad.

Allaan alikamatwa kwa kuhusishwa na kundi la kiislamu la Islamic Jihad.

Idara ya magereza Israel inaarifiwa kukataa ombi la kumuachilia huru kwa misingi ya kuzorota kwa hali yake ya afya.