Mlipuko China:Watu 95 hawajulikani waliko

Haki miliki ya picha EPA
Image caption 95 hawajulikani waliko nchini China

Siku nne baada milipuko mikubwa kuukumba mji wa Tianjin nchini China, utawala unasema kuwa bado watu 95 hawajulikani waliko.

Karibu wale wote wasiojulikana waliko ni wazima moto.

Idadi ya watu waliouawa kwenye milipuko hiyo imepanda hadi zaidi ya watu 110.

Wasimamizi wa mitaandao nchini China wamefunga mitandao kadha inayodaiwa kuzua hofu kwa kuchapisha habari zisizokuwa za kweli.

Mapema mamia ya mitandao ya kijamii ilifungwa na utawala kwa kueneza uvumi kuhusu milipuko hiyo.