Kitabu cha kuchuja maji chagunduliwa

Haki miliki ya picha WATERISLIFE KRISTINE BENDER
Image caption Kitabu cha kuchuja maji chagunduliwa

Kitabu chenye kurasa ambazo zinaweza kuraruliwa na kisha kutumiwa kuchuja maji ya kunywa kimepata mafanikio katika majaribio yake ya kwanza.

Kitabu hicho pia kina maandishi ya ujumbe kuhusu jinsi maji yanaweza kuchujwa. Kurasa za kitabu hicho zina kemikali maalum ambayo huua viini vilivyo kwenye maji wakati maji yanapochujwa kwa kutumia kurasa zake.

Majaribio 25 kwenye maji machafu nchini Afrika kusini , Ghana na Bangladesh, karatasi kutoka kwa kitabu hicho zilifanikiwa kuondoa asilimia 99 ya viini kutoka kwa maji hayo.

Ubora wa maji ulipatikana baada ya kuchujwa kwa maji machafu ulifikia viwango vya ubora wa maji ta mfereji nchini Marekani

Dr Teri Dankovich ambaye ni mtafiti katika chuo cha Carnegie Mellon mjini Pittsburg aliunda na kujaribu teknolojia ya kitabu hicho kwa miaka mingi.

Haki miliki ya picha Teri Dankovich
Image caption Kitabu cha kuchuja maji chagunduliwa

Teknolojia hiyo itatumiwa na jamii kwenye nchi zinazoendelea."Watu milioni 663 kote duniani hawapati maji safi ya kunywa" alisema Dr Dankovich.

Anasema kuwa kile mtu anahitaji kufanya ni kurarua kitabu na kuweka karatasi na kuitumia kuchuja maji ambayo hutiririka yakiwa masafi na yasiyo na viini.

Dr Dankovich tayari ameifanyia majaribio katarasi hiyo katika mahabara akitumia maji yaliyochafuka.

Baadaye aliifanyia majaribio akitumia maji machafu ambayo yamechafuka kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili iliyopita ambapo ilipata mafanikio makubwa.