Vijana wachangia damu wanajeshi Cameroon

Image caption Mchango wa VIjana nchini Cameroon katika mapambano dhidi ya Boko haram ni kuchangia wanajeshi Damu

Mamia ya vijana nchini Cameroon,wamejitolea kuwapa damu wanajeshi wanaopambana na kundi la Boko Haram kaskazini mwa nchi hiyo.

Kampeni hiyo imeandaliwa na baraza la muungano wa vijana nchini humo. Wanasema, huu ndio mchango wao dhidi ya ugaidi.

Hospilitali ya kijeshi ya Yaounde ambayo wanajeshi waliojeruhiwa kutoka Cameroon na Chad hupewa matibabu, imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa akiba ya damu ya kutosha .

Lakini kutokana na jitihada za vijana hao sasa akiba ya damu imeanza kuongezeka.