Mchezo wa ng'ombe wawaua watu 7 Uhispania

Haki miliki ya picha epa
Image caption Matadoo

Ng'ombe wanaotumiwa katika mchezo wa Matador wamewaua watu saba katika sherehe nchini Uhispania tangu mwanzo wa mwezi Julai huku wanne wakiuawa wikendi iliopita.

Vifo hivyo vilitokea wakati wa kufukuzana na ng'ombe hao katika barabara na sio ndani ya ukumbi wa mchezo huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Matadoo

Ni idadi kubwa ya vifo iliorekodiwa katika mda mfupi.

Miongoni mwa waliouawa ni diwani mmoja mwenye umri wa miaka 36 aliyeuawa katika mji wa Penafiel,mji ulio karibu na ule wa Valladolid kaskazini mwa Madrid.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ngombe

Kaskazini zaidi kijana mwenye umri wa miaka 18 alidungwa kwenye tumbo na ng'ombe na kufariki katika eneo la Lerin huko Navarra.

Vifo vyengine vilitokea wakati wa sherehe za ngombe katika majimbo ya Valencia,Murcia,Toledo,Castellon na Alicante.